BBC navigation

Kasri yageuka kambi ya waasi CAR

Imebadilishwa: 10 Februari, 2014 - Saa 08:41 GMT

Mfalme Bokasa CAR

  • Vurugu zilizozuka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, hazijasaza kasri ya kifahari ya aliyekuwa mfalme Bedel Bokassa. Maji ya bwawa hili yamegeuka na kuwa kijani.
  • Katika miaka 35 tangu Bokassa kuong'olewa mamlakani, kasri imeharibika sana na kwa sasa imevamiwa na mamia ya wapiganaji. Makurutu hawa wanaobeba silaha za ambao walitelekezwa na makamanda wao wakati waasi wa Seleka walipochukua mamlaka.
  • Wakati wa utawala wa Bokassa miaka 14 iliyopita, alituhumiwa kwa kula watu huku akiwalisha maadui wake nyama ya Simba na Mamba katika hifadhi yake ya wanyama.
  • Mwaka 2010, Rais Francois Bozize, aliyeondolewa mamlakani mwezi Machi, aliwahi kumpa hifadhi mfalme Bokassa hasa katika siku ambayo alitawazwa hapa akivalia mavazi yaliyoigwa kutoka kwa Napoleon.
  • Peter Bouckaert, kutoka kwa shirika moja la kutetea haki za binadamu, aliyezuru kasri la Bokassa, alisema kuwa makurutu katika makundi ya wapiganaji wanaishi katika kasri hiyo kwa sababu wanaogopa sana wanaweza kusemekana kuwa waasi.
  • Wapiganaji hao wamekuwa wakiishi katika eneo hilo bila chakula. Hapa wanaonekana wakiomba chakula.
  • ''Nilihisi tofauti sana kutembea katika kasri hii na kuona wapiganaji wakiwa na silaha bandia.'' alisema bwana Bouckaert.
  • Kikundi cha wanaharakati kilikuwa kinaelekea nje ya mji wa Boda umbali wa kilomita 180 kutoka mji mkuu Bangui kilipoona kasri hiyo. Safari yote kuelekea Boda, ilichukua muda wa masaa tano.
  • ''Tulipofika mjini , tulipata maelfu ya raia waliokuwa na hofu kubwa wakijificha majumbani mwao kutokana na makabiliano makali katika siku nne zilizopita. Raia wanaomba wanajeshi wapelekwe katika eneo hilo. Waisilamu wanaokabiliwa na tisho la usalama wamebakia kujihami kwa nyuta na mishale
  • Makabiliano kati ya wakristo na waisilamu yalianza baada ya waasi wa zamanai wa Seleka ambao walimsaidia rais wa zamani Michel Djotodia kuingia mamlaknai na kuwa Rais wa kwanza muisilamu kushika hatamu. Lakini aliondoka madarakani kama sehemu ya makubaliano ya kutafuta amani

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.