BBC ilivyomuenzi Komla Dumor

23 Januari 2014 Imebadilishwa mwisho saa 09:13 GMT

Tunatoa rambi-rambi zetu maalum kwa mtangazaji mwenzetu mahiri barani Afrika.

Komla Dumor mtangazaji wa BBC Idhaa ya Dunia na Focus on Afrika alifariki siku ya Jumamosi kutokana na mshituko wa moyo.

Rambi-rambi nyiingi zimekuwa zikimiminika kutoka kwa Watazamaji na wasikilizaji wetu tokea wasikie habari za kifo chake.

Lakini limekuwa pigo kubwa sana kwetu. Hasa familia ya Focus on Afrika na Dira TV, kwa sababu Komla hakuwa tuu mfanyakazi mwenzetu lakini alikuwa ni rafiki pia.