Unajivunia Kinyozi wako?

20 Januari 2014 Imebadilishwa mwisho saa 09:27 GMT

Maonyesho ya vinyozi kadhaa vilivyo katika mataifa kadhaa Afrika yanaendelea mjini London. Nini hukuvutia katika kinyozi chako?
Maonyesho yaliyofanywa mjini London ya mpiga picha mnigeria Andrew Esiebo kuangazia vinyozi katika miji 8 barani Afrika
Majivuno ndio kauli mbiu ya mifumo ya kunyoa nywele ambayo maduka mengi ya vinyozi huwa nayo katika miji ya Lagos, Cotonou, Abidjan, Monrovia, Bamako, Dakar, Nouakchott na Accra.
Mradi huu wa Esiobo, unahusisha mambo kadhaa yanatokamana na vinyozi na ambyo yanayohusiana na ambayo hutumiwa kama vitendawili kuzungumzia wanaume wa kiafrika ndani ya vinyozi
Vinyozi hutaka kuwagusa sana wanaume kwa kutumia mitindo tofauti kukata nywele zao na kuwafanya kukaa wanavyotaka wenyewe wakiwa na mvuto wa asili ya kiafrika. Ndio njia yao ya kuwavutia wateja
Duka hili la Kinyozi ni moja ya vinyozi vinavyoleta taswira ya maduka ya vinyozi vya kisasa katika miji mingi tu Afrika
Kila kinyozi kina muundo na mvuto wake wenye lengo la kuleta wateja
Maonyesho haya ya maduka ya vinyozi yataendelea hadi tarehe 8 Februari mwaka 2014 mjini London