BBC navigation

Mustakabali wa misri kwenye mizani

Imebadilishwa: 16 Januari, 2014 - Saa 19:50 GMT

Katiba mpya Misri

  • Kwa siku mbili zijazo, Wamisri watajua ikiwa watakuwa na katiba mpya au ikiwa rasimu ya katiba inayopigiwa kura haitaidhinishwa.
  • Nchi hii imekuwa ikikumbwa na hali ngumu ya kisiasa tangu mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani Hosni Mubarak.
  • Baadhi walihisi huo ndio ulikuwa mwisho wa siasa mbaya lakini baadaye rais aliyechaguliwa kihalali Mohammed Morsi, aliondolewa mamlakani na jeshi
  • Morsi alikuwa mwanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo ikiwa katiba hii itapitishwa ndio itakuwa mwisho wake. Chini ya Katiba mpya Vyama haviwezi kuundwa kwa misingi ya kidini, kabila, jinsia na kijiografia. Bila shaka itakuwa pigo kubwa kwa vuguvugu la Muslim Brotherhood
  • Misri pia imekuwa ikikumbwa na hali mbaya ya usalama. Mashambulizi ya kulipiza kisasi na ya kuvizia yakiwa jambo la kawaida. Chini ya katiba hii waziri wa ulinzi sharti awe mwanajeshi kama hali ilivyo sasa.
  • Ulsama ulidhibitiwa kote nchini humo kwa hofu ya mashambulizi
  • Wake kwa waume, wazee kwa vijana wote walijitokeza kwa hamu ya kuipatia Misri mustakabali mwema wa kisiasa

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.