BBC navigation

Ajira baharini Sierra Leone

Imebadilishwa: 8 Januari, 2014 - Saa 15:44 GMT
 • Klabu ya wachezaji wa mchezo wa kuteleza kwenye mawimbi ya maji kwa kibao kijijini Bureh kilizinduliwa kama shirika lisilo la kiserikali ambalo nia yake ilikuwa kuimarisha mchezo huo nchini Sierra Leone na pia kutoa nafasi za kazi kwa watu wa kijiji hicho. Kwa sasa hii ndio klabu ya kwanza na ya kipekee ya aina yake Sierra Leone.
 • Hadi miaka mitatau iliyopita, wachezaji wa klabu ya Bureh hawakujua mbinu za mchezo huu zinazotumiwa na watu kwingineko duniani
 • Watu wengi kijijini humo walijifunza mchezo wa kuteleza kwa mawimbi ya maji wakitumia vibao walivyoazima kutoka kwa wageni waliokuwa wanatembelea bahari. Sasa klabu hii inamiliki vibao ambavyo hivikodisha kwa watu wanaotaka kuvitumia
 • Jahbez ambaye alikuwa mvuvi alikuwa mmoja wa walioanzisha klabu hiyo .'' Haikuwa kazi rahisi , wakati mwingine ungetoka kutafuta vibao wala hupati kitu. Sasa haya ni maisha mazuri kwangu.''
 • K-K ni mchezaji wa kwanza mwanamke wa kuteleza kwa mawimbi ya maji kwa kutumia vibao Siera Leone. ''Wengine wanaogopa. Hawajui kuogelea'' Lakini ikiwa utajitolea kujifunza , unaweza kufanya lolote. '' Anasema K.K
 • 'Kuna sehemu moja hapa baharini ambapo huwezi kukosa mawimbi.'' anasema mpenzi wa mchezo huu mwenye uraia wa Irelend, Shane O'Connor ambaye alisaidia vijana wa klabu hiyo kuanzisha klabu yao.
 • Kwa sasa wateja wa klabu hiyo ni wageni wa kimataifa wanaoishi mjini Freetown. lakini sasa watu wengi wanazuru nchi hiyo mchezo huu ukiwa kichocheo cha ziara yao.
 • Peter Wessels, amekuja kuteleza hapa mara mbili sasa na anapendezwa na ambavyo klabu hiyo inafanya kazi na pia ambavyo hushughulikiwa kama mteja
 • O'Connor anasema kuwa lengo lao ni kuwa na shirika ambalo litatoa motisha kwa vijana kujihusisha na mchezo huu.
 • Klabu hiyo inafanya kazi vyema kiasi cha kuwavutia watu kutoka Sierra Leona na hata wageni wa kimataifa. Pia kuna juhudi za kutaka kujumuisha nchi hiyo kama mwanachama wa shirikisho la kimataifa la mchezo huu
 • Miaka 11 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sierra Leone, taifa hilo lingali linajitahidi kuinua sura yake na sifa yake kimataifa kupitia kwa sekta ya utalii. Picha za Tommy Trenchard

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.