BBC navigation

Picha zilizotesa mwaka 2013

Imebadilishwa: 2 Januari, 2014 - Saa 10:02 GMT

Picha za mwaka

  • Kutekwa kwa mji wa Konna nchini Mali kulisababisha Ufaransa kupeleka wanajeshi wake huko kushika doria...hali hii ndiyo ilimpa furaha isiyo na kifani mtu huyu kwani waasi walikuwa wameweka sheria za kiisilamu zilizoharamisha mambo mengi
  • Timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles ndiyo iliyowaondoa mashabiki hawa kutoka katika viti vyao baada ya kushinda kombe la taifa bingwa Afrika. Kombe hilo lilikuwa limewakwepa kwa miaka 13
  • Zimbabwe ilikwenda kwenye debe mara mbili, kupigia kura kura ya maamuzi na uchaguzi mkuu. Mugabe ndiye aliyeshinda na huyu ni mmoja wa mashabiki wake
  • Nchini Afrika Kusini mambo yalikuwa mitindo mipya na ya kisasa kwenye mashindano ya mitindo ambayo vijana hawa walishiriki.
  • Eneo la Mashariki mwa Congo lilivamiwa na waasi wa M23 kwa karibu mwaka 2013 wote, lakini mwishoni baada ya juhudi nyingi za jeshi la DRC na UN waasi hao walisalimu amri baada ya kupata kipigo kikali.
  • Mnamo mwezi Juni, jeshi la Senegal lilimkaribisha Rais Barack Obama kwa ziara yake ya Afrika akianzia nchini humo na kisha kuelekea Afrika Kusini na Tanzania.
  • Shambulizi la kigaidi lilikumba Kenya mwezi Septemba ambapo watu zaidi ya sitini na tano waliuawa baada ya wanamgambo wa Al shabaab kuteka jengo la westgate kwa zaidi ya siku tatu
  • Maombi yalifanywa kote nchini humo hali ilipozidi kuwa mbaya
  • Disemba dunia iliomboleza kifo cha hayati Nelson Mandela alipofariki akiwa na umri wa miaka 95.Alizaliwa kijijini Qunu na alizikwa tarehe 15 mwezi Disemba.
  • Mjane wa Mandela Garaca Machel na aliyekuwa mke wa Mandela Winnie Mandela wakiomboleza kifo cha mzee Mandela wakati wa mazishi ya shujaa huyo wa Afrika

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.