BBC navigation

Mandela afanyiwa ibada Maalum

Imebadilishwa: 10 Disemba, 2013 - Saa 15:35 GMT

Mandela Service

 • Melfu ya watu nchini Afrika Kusini walijiunga na zaidi ya viongozi 90 wa dunia kwa ibada maalu ya hayati Nelson Mandela.
 • Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa michezo wa FNB mjini Johannesburg
 • Rais wa Marekani Barack Obama alisema kuwa Mandela ameifunza dunia umuhimu wa kutenda badala ya kusema sana pamoja na umuhimu kwa kuwa na mawazo mazuri ingawa ya kutenda.
 • Alipoondoka ukumbini, Rais Obama aliamkuana na Rais wa Cuba, Raul Castro ishara kubwa sana kati ya marais wa nchi hizo mbili ambazo zimekuwa zikizozana kwa zaidi ya nusu karne
 • Mandela alifariki Alhamisi iliyopita, akiwa na umri wa miaka 95. Nchi hiyo imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya kuzikwa Jumapili.
 • Aliyekuwa anaendesha hafla hiyo Cyril Ramaphosa alisema kuwa safari ndefu ya Mandela imekamilika na sasa anaweza kupumzika
 • Askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu,mmoja wa waliopigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, alisema Mandela alikuwa mtu wa kupatanisha watu pindi alipoondoka gerezani. 'Tumepata afueni kuwa matatizo yake ya kiafya yamekwisha' alisema Tutu
 • Ibada hii ilikuwa moja ya mkusanyiko mkubwa wa viongozi wa dunia kushuhudiwa hivi karibuni. Katika hotuba yake , katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki Moon, alisema kuna huzuni tele kwa umma kumpoteza Mandela
 • Kulikuwa na hofu kuwa watu wangeamrishwa kurejea nyumbani , lakini mvua kubwa ilisababisha sehemu za uwanja kuwa bila watu
 • Mjane wa Mandela Graca Machel, alishangiliwa sana alipoonyeshwa kwenye skirini kubwa akiingia uwanjani
 • Pia kulikuwa na shangwe na vigelegele huku watu wakiimba Winnie Winnie Madikizela Mandela aliyekuwa mkewe Mandela. Alimpa pambaja na kumbusu Graca
 • Hata hivyo Rais Jacob Zuma alizomewa mara kwa mara ilipokuwa zamu yake kuhutubia wananchi.
 • Tangu kifo cha Mandela mji wa Johannesburg umekuwa ukishuhudia mvua lakini hiyo haikuwakatiza tamaa wananchi waliofurika uwanja wa michezo wa FNB
 • Umati wa watu uliimba na kucheza kama ishara ya kuenzi maisha ya Mandela
 • Ambao hawakuweza kufika uwanjani waliiona ibada hiyo kwenye televisheini zao nyumbani kote nchini Afrika Kusini
 • Mandela atazikwa siku ya Jumapili tarehe 15

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.