Jaji Joseph Warioba amkumbuka Mandela

8 Disemba 2013 Imebadilishwa mwisho saa 11:19 GMT

Watu waliomfahamu Mzee Nelson Madiba Mandela wameendelea kumuelezea namna walivyomfahamu enzi za uhai wake.

Nchini Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba ni miongoni mwa watu waliomfahamu Nelson Mandela kwa karibu kutokana na kufanyakazi pamoja ukiwemo wakati wa kushughulikia mgogoro wa Burundi.

kwenye mahojiano na Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam, Leonard Mubali,Jaji Warioba anaanza kuuelezea alivyopokea msiba huo na kisha kumuelezea Mandela ni nani