Maandalizi ya Sema Kenya

17 Novemba 2013 Imebadilishwa mwisho saa 14:03 GMT

Sema Kenya kinaandaliwa kwa makini na ubora wa hali ya juu.
Sema Kenya ni kipindi cha mjadala kinachoangazia maswala ya utawala na maendeleo.
Kipindi hiki kinahakikisha wananchi wa kawaida wanapata jukwaa la kuuliza viongozi wao maswali tata, ana kwa ana.
Utafiti na ubora wa kipindi ni wa hali ya kipekee.
Kipindi kimeweza kutamba kote nchini kutokana na utaalam ulipo kwenye uandalizi.
Muda mwingi unatumiwa kurekodi na kusimulia kipindi hiki ili kueleza mambo kama yalivyo.
Kila kinapopeperushwa, kipindi hiki kinazidi kuboreshwa ili Wakenya wazidi kujadiliana na viongozi wao, kusudi utawala bora ufikiwe.