Kwaheri Sachin Tendulkar!

15 Novemba 2013 Imebadilishwa mwisho saa 08:26 GMT

Alijulikana kama 'Maximum City' na sasa Mashabiki wake nchini India wamemuaga Sachin akisema Kriketi tosha!
Anajulikana kama 'Maximum city' na mwandishi vitabu maarufu sana. Lakini leo Sachin Tendulkar anaaga mchezo wa kriketi mbele ya maelfu ya mashabiki wake nchini India.
Huyu ni kakake aliyefika uwanjani kusherehekea naye na kumuaga kutoka katika kriketi
Tendulkar ni mchezaji maarufu zaidi wa Kriketi nchini India baadhi wakisema ubingwa wake unafikia kiwango cha kuwa mchezaji bora zaidi duniani wa kriketi
Sachin alikabidhiwa fursa ya kuweza kuwaleta jamaa zake wote katika uwanja huu kushuhudia mechi yake ya mwisho kabla ya kuacha rasmi mchezo huu. Huyu ni kakake pamoja na kocha wa Sachin aliye kwenye kiti cha magurudumu
Waliokuwa wanakwenda kumuona Sachin akicheza mchezo wake wa mwisho, walighadhabishwa mno na fursa aliyopewa ya kuwaalika jamaa na marafiki mia nne kwani hawakununua tiketi za kuona mechi hiyo. Huyu hapa ni bintinye
Sachin ana mashabiki maelfu vijana , wazee akina mama, watoto na wote wanaomtambua tu hata kwa picha
Mamia ya watu walipiga foleni kununua tiketi za kuwjionea mchezo wa mwisho a Sachin katika ardhi ya India na kumuaga bingwa wao wa kriketi.
Mashabiki sio wazee tu wambo wameuona Sachin akicheza kriketi kwa zaidi ya miongo miwili, watoto pia wamo.
Usalama ulidhibitiwa kote mjini Mumbai tayari kwa mchuano wa mwisho wa kriketi ambao Tendulkar alishiriki.
Kila mahali kulikuwa na mabango, fulana, na kila ishara ya watu nchini India kumuenzi Tendulkar
Kwa sasa kuna hoja ikiwa Tendulkar anaweza kutajwa kuwa mchezaji bora zaidi wa Kriketi duniani, raia wengi wa India bila shaka wataiona hiyo kuwa kweli kabisa.