BBC navigation

Afrika wiki hii kwa picha

Imebadilishwa: 21 Oktoba, 2013 - Saa 15:40 GMT

Picha za wiki Afrika

  • Watoto hawa walipigwa picha siku ya Jumatatu nchini Lesotho katika eneo la milimani la nchi hiyo, kabla ya sherehe ya ufunguzi wa shule moja ya wavulana ya Herd katika eneo la vijijini la Mateanong iliyojengwa na shirika lisilo la kiserikali la Sentebale, lililoanzishwa na Prince Seeiso wa Lesotho
  • Mnamo siku ya Jumamosi mashabiki wa soka wa Algeria na Burkinabe wanawashabikia timu zao katika mkondo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kushiriki kombe la dunia mjini ,Ouagadougou Burkina Faso’s. Stallions waliwashinda mahasimu wao mabao 3-2.
  • Mahujaji wanawake wa kiisilamu wanapiga picha katika mlima wa toba wa Arafat karibu na mji mkuu Mecca nchini Saudi Arabia siku ya Jumatatu wakati wa siku ya mwisho ya Hajj.
  • Mtoto mvulana anaonekana hapa kwenye maombi ya Eid mjini Abidjan, Ivory Coast – siku ya Jumanne tarehe 15 Octoba 2013
  • Siku hiyo hiyo nchini Nigeria, ambako wanamgambo wa kiisilamu wanapigana dhidi ya serikali, polisi mmoja anasimama wima kuweka usalama wakati wa sala ya Idd katika uwanja mmoja ambako watu walifanyia maombi mjini Abuja.
  • Siku iliyofuata, waisilamu walisherehekea siku kuu ya Eid al-Adha, ambayo pia inajulikana kama Tabaski, kwa kuchinja mbuzi kama ishara ya kutoa kafara kwa sababu ya kuwapa nyama watu maskini wasio na chakula
  • Wakati wa sherehe za Eid, mjini Mogadishu, watoto wanacheza kwenye vifusi, vya majengo wakiwa na bunduki bandia.Walipokea bunduki hizi bandia kama zawadi ya Idd.
  • Siku hiyo hiyo, katika bandari ya Benghazi nchini Libya , mtu huyu mwenye hasira na ambaye alishiriki katika maandamano, ya kupinga kitendo cha serikali ya Marekani cha kumkamata raia mmoja wa nchi hiyo baada ya kushukiwa kuwa gaidi, hapa anaoenkana akiteketeza bendera ya Marekani.
  • Wacheza dansi, wanajipaka rangi kwenye nyuso zao wakati wa sherehe moja katika uwanja wa kriketi mjini Cape Town,kwenye tamasha la Holi. Holi, ni tamasha la rangi na huashiria mwisho wa msimu wa baridi, na hasahasa hupendwa zaidi katika jamii za kihindi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.