Afrika kwa picha

7 Oktoba 2013 Imebadilishwa mwisho saa 09:50 GMT

Wavuvi wa pweza Tanzania na wakimbiaji Berlin katika mkusanyiko wa picha kutoka sehemu mbali mbali Afrika
Mshindi wa mbio za Marathon mjini Berlin, Ujerumani mkenya Wilson Kipsang mwenye umri wa miaka 31. Hapa anasherehekea ushindi wake. Alivunja rekodi ya mbio hizo kwa sekunde kumi na tano.
Wachezaji wa mchezo wa Roller Skating mjini Lagos Nigeria wanasherehekea miaka 53 ya uhuru wa Nigeria.
Watoto wa shule pia walisherehekea uhuru wa Nigeria kote nchini humo siku ya Jumanne wiki jana
Wafanyakazi wakibeba mchanga kutoka machimboni mjini Mogadishu,siku ya Jumanne. Kuna machimbo mengi kama hay ambayo yamekuwa na shughuli nyingi katika miaka miwili iliyopita tangu al-Shabab kufurushwa na kusababisha ujenzi mkubwa.
Msichana huyu alikuwa miongoni mwa waliohudhuria maombi maalum kwa watu waliofariki kutokana na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la Westgate mjini Nairobi, Kenya
Raia hawa wa Ghana walihudhuria kongamano la kila mwaka la chama cha Conservative katika mtaa wa Manchester nchini Uingereza
Carranzar Naa Okailey Shooter, (kushoto) aliwakilisha Ghana katika mashindano ya mwanamke mrembo zaidi duniani. Hapa amesimama na mshindi wa mashindano hayo (katikati) kutoka Ufilipino.
Wamiliki wa boti za usafiri wanawasubiri abiria kwenye fuo za mto Nile mjini Cairo. Safari za boti ni jambo la kawaida sana na watu husafiri kwa boti zaidi nyakati za jioni kujivinjari
Mvuvi nchini Tanzania anatazama akiona mitumbwi ya kuvua samaki na wavuvi wakiwasili kutoka baharini asubuhi na mapema.
Pindi wanapowasili, wavuvi hukimbia sokoni na samaki wao waliowavua kwa siku hiyo kuelekea kuwauza katika soko la Kivukoni
Si Samaki pekee wanaovuliwa bali pia Pweza hawa wanaoaminika kuongeza nguvu za kiume mwilini
Uhaba wa maji nchini Senegal ni tatizo sugu na hii ndiyo dalili yake watu kupanga foleni kununua maji