Huwezi kusikiliza tena

Microsoft yanunua Nokia

6 Septemba 2013 Imebadilishwa mwisho saa 07:45 GMT

Iliyokuwa kampuni kubwa zaidi ya kutengeza simu za mkononi, Nokia, imenunuliwa na kampuni ya Microsoft. Kampuni ya Nokia ambayo imwkuwa ikikabiliwa na changamoto za kifedha, ilitupilia mbali mfumo wake na kuasili ule wa Windows katika juhudi za kutaka kujikwamua kifedha.