Maisha vitani Jamuhuri ya Afrika ya Kati

21 Agosti 2013 Imebadilishwa mwisho saa 19:40 GMT

Maisha ya raia wengi Jamuhuri ya Afrika ya Kati yamekua ya kuhangaika katika kijiji kimoja kinachothibitiwa na waasi wa LRA
Cimene Kpalanale na mwanawe katika kituo cha afya kinachofadhiliwa na shirika la Merlin
Chimene Kpakanale ni mama wa miaka 22. Yeye ana bahati ya kujifungulia mwanawe wa kiume hospitalini, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati. Akina mama wenzake wamelazimika kuzalia wanao kambini au vichakani kufuatia mapigano nchini humo.
Chimene na Mwanawe, wajifunika kujikinga jua laki
Jamuhuri ya Afrika ya Kati imetajwa miongoni mwa nchi zinazoongoza katika vifo vya watoto. Mtoto mmoja kati kumi hufariki dunia kabla ya kufikisha umwi wa mwaka mmoja. Usalama umekua mbaya Jamuhuri ya Afrika ya Kati kufuatia, mapinduzi yaliyofanywa na waasi wa Seleka dhidi ya serikali ya Rais Francoise Bozize.
Chimene Kpakanale anawaonyesha jirani zake mwanawe aliyejifungua
Bi Kpakanale na mumewe wana watoto watatu na wanaishi eneo la Obo. Eneo hili limekua ngome kuu ya waasi wa Uganda wa LRA wanaoongozwa na muasi Joseph Kony. Hapo mwezi Machi LRA walishambulia eneo hilo.
Watoto wakicheza nje ya makaazi moja Jamuhuri ya Afrika ya Kati
Raia wengi wamekimbia mapigano katika mji mkuu Bangui na kuingia eneo la Obo. Kutokana na raslimali chache, maisha ya wengi hapa yamekua ya kuhangaika kila uchao.
Mtoto aliya na tatizo la utapya mlo
Kusini Magharini mwa Nchi, kunashuhudiwa mfumuko wa bei ya vyakula. Aidha viwango vya utapya mlo vimekithiri. Muuguzi wa kiume Anatole Nzu amekua akiwahudumia wakimbizi katika kambi iliyoko eneo la Batalimo, karibu na mapaka na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Muuguzi Anatole Nzu akimhudumia mgonjwa katika kituo cha shirika la Merlin
Uporaji na mashambulio ya mara kwa mara yamepeleka wahudumu wa misaada kukimbia. Hata hivyo muuguzi Nzu ameamua kusalia eneo hilo kuendelea kuwahudumia wagonjwa wengi ambao huwa ni majeruhi wa mashambulio ya waasi wa Seleka.
Muuguzi Anatole Nzu akimbeba mgonjwa
Kwa wakati mmoja kituo hiki kilikumbwa na uhaba mkubwa wa dawa. Hali mbaya ya usalama ililazimisha magari ya kutoa misaada kuhifadhiwa katika nchi jirani ya DRC
Wagonjwa wakisubiri huduma ya afya katika kituo cha Merlin
Miezi sita baada ya waasi wa Seleka kuipindua serikali, muuguzi Nzu ameshuhia ongezeko la wagonjwa wanaofika kituo chake kutafuta huduma ya afya. Wengi hufika saa moja kabla ya kituo kufunguliwa
Muuguzi kutoka Congo Anatole Nzu na familia yake
Bw. Nzu aliwasili eneo la Batalimo kutoka nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo alitoroka mapigano.Kwa sasa anaishi kwa nyumba hii ya matope akiwa na mkewe na wanawe wanne.
Baadhi ya wakimbizi katika kambi la Batalimo, Jamuhuri ya Afrika ya Kati
Takriban watu milioni 4.6 raia wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji msaada wa dharura. Hawana maji safi, chakula, huduma ya afya wala makaazi. Mshirikishi wa kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos amesema raia wengi wanaishi kwa matawi ya msituni kama chakula cha kila siku.
Mwanawe Chimene Kpakanale
Shirika la kutoa misaada la Merlin limeonya ongezeko la vifo vya watoto katika nchi hiyo. Aidha kuna tisho la kuzuka janga la kibinadamu. Waasi wa Seleka wamekua wakipora mali ya watu na maafisa wa Umoja wa Mataifa wanaomba kutumwa jeshi la kulinda amani ili kurejesha uthabiti katika taifa hilo la Afrika ya Kati
Jacob Zocherman mhudumu wa Merlin akitoa chanjo
Bi Kpakanale alijifungua mwanawe wa kiume hapo Julai 17. Kabla ya kuondoka hospitalini alipokea chanjo dhidi ya kifua kikuu na kupooza.Mhudumu wa shirika la Merlin Jacob Zocherman amesema uhaba wa chanjo umepelekea kulipuka maradhi ya ukambi na tetekuwanga.