BBC navigation

Afrika kwa picha

Imebadilishwa: 13 Agosti, 2013 - Saa 14:50 GMT

Wiki hii picha

 • Mashua ya uvuvi kwenye ufuo wa bahari katika mji mkuu wa Senegal , Dakar ikielekea baharini siku ya Jumanne ambako boti moja iliharibika na kuvuja mafuta. Hali ingali kudhibitiwa na tayari imezua wasiwasi kuhusu uharibifiu wa mazingira
 • Katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, siku hiyo ya Jumanne mtoto akitembea na bunduki bandia kwenye ufuo wa bahari ya Lido
 • Mwogeleaji wa Ghana mtindo wa butterfly Ophelia Swayne akishindana kwenye mashindano ya uogeleaji yaliyokamilika nchini Spain Ijumaa. Hakushinda medali yoyote ingawa aliweza kuogelea kwa muda wake bora zaidi.
 • Familia ambazo nyumba zao ziliharibiwa kwenye mafuriko mjini, Khartoum, wanapumuzika kwenye vitanda vyao kando ya barabara Jumanne. Mashirika ya misaada yalisema kuwa watu 11 walifariki na wengine 98,500 wameathiriwa na mafuriko hayo ambayo chanzo chake ni mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha tangu tarehe moja hadi nne mwezi huu
 • Mwanamke nchini Zimbabwe akianika nguo zake baada ya rais Mugabe kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi jana
 • Mnamo siku ya Jumapili, kijana huyu anaonekana akicheza na mpira katika kambi ya watu walioachwa bila makao kufuatia mapigano katika mkoa wa Kivu Kaskazini karibu na mji wa Goma
 • Siku mbili baadaye mama huyu anaanda Ugali katika mji katika kambi nyingine karibu na mji wa Goma
 • Mwanamume mmoja Mashariki mwa mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria anapuliza ala yake ya muziki wakati wa sherehe za Idd
 • Mji wa Maiduguri ni kitovu cha harakati za Boko Haram na hii ndio mara ya kwanza kwa sherehe za idd kufanyika mjini humo tangu kundi hilo kuanza harakati zake
 • Mkewe rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Winnie Mandela kitia siani kitabu chake cha hivi karibuni
 • Mwanamke anawaelekeza vipofu watatu ambao huimba wakati wakiomba pesa katika soko moja mjini Bamako, Mali

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.