William na Kate warejea nyumbani

24 Julai 2013 Imebadilishwa mwisho saa 09:46 GMT

Mwanamfalme wa Uingereza William na mkewe Kate wamerudi nyumbani na mtoto wao wa kwanza wa kiume.
Mkewe mwanamfalme wa Cambdridge Prince William alionekana akicheka na kufurahia huku akiodnoka katika hospitali ya St Mary's mjini London. Hapa yuko na mumewe
Mtoto alionekana kutoa salamu zake za kwanza za kifalme naye akiamkuliwa na watu wengi tu wlaiokuwa nje ya hospitali hiyo kumpokea
Babake mtoto Prince William alisema bado hawajampa mwao jina
Akimpakata mwanawe, mkewe mwanamfalme Kate ,alisema ni siku muhimu sana kwa maisha mama yeyote yule
Wazazi wawili walisema kumpata mtoto huyo lilikuwa jambo lililoleta hisia kubwa sana
Prince William alimpakata mwanawe mwenyewe kabla ya kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari
Wazazi hao wapya walifichua kuwa baba ndiye aliyembadilisha mtoto nepi yake ya kwanza
William ndiye alimuingiza mwanao ndani ya gari kabla ya kuondoka
Wote wlaielekea nyumbani katika kasri la Kensington gari likiendeshwa na William mwenyewe
Sio mara ya kwanza kwa William kupigwa picha akiwa katika hospitali ya St Marys , katika picha hii amepekatwa na mamake, marehemu Diana, punde baada ya kuzaliwa katika hospitali hiyo