BBC navigation

Wazima moto wa Freetown

Imebadilishwa: 23 Julai, 2013 - Saa 11:59 GMT

Wazima moto

 • Esther Magati anasubiri simu ya dharura katika kituo rasmi cha wazima moto katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown. Wapiga simu wanaweza tu kuwasiliana na kupata msaada ikiwa simu zao zinatumia mtandao wa Africell
 • Kikosi cha wazima moto pia kinakabiliwa na changamoto za upungufu wa maji. Wakati lori la kubeba maji linapotumia maji yake litalazimika kusafiri umbali mkubwa sana kuteka maji mengine kabla ya kurejea kuendelea kuzima moto.
 • Licha ya kuwepo upungufu wa maji, miongoi mwa majukumu yao ni kunyunyizia maji bustani la rais katika ikulu yake wakati wa hafla rasmi za serikali
 • Afisaa mkuu wa wazima moto, Naziru Bongay alisema kuwa asilimia 60 ya nyumba zimejengwa kwa mabati, vijiti na mbao, na wakati unapoangalia vifaa hivyo vyote vilivyotumiwa kwa ujenzi, nyumba hizi tunaziita mitaa ya mabanda, moto ni rahisi sana kuziteketeza
 • Mioto inayokatana na hitilafu za nyaya za stima, ni kawaida sana nchini Sierra Leone, ambako ubovu wa kuweka nyaya hizo pamoja na moto mwingi wa stima kupita kiasi husababisha moto katika makao haya.
 • ''Jiografia ya Freetown na msongamano wake mkubwa wa nyumba, maeneo ya ufuo, milimani na maeneo mengine, ambako hakuna barabara nzuri za usafiri huwa changamoto kubwa sana wakati moto unapozuka, '' asema bwana Bongay
 • Wakati huu ambapo kumekuwa na kiangazi, kikosi cha wazima moto ambacho huhudumia mji wa Freetown, ...Wenye idadi ya watu milioni 1.2 huwa na gari moja tu lenye vifaa vinavyohitajika wakati wa kuzima moto, baada ya magari mengine mawili kuharibika. Kumekuwa na wakati mgumu sana
 • Mzima moto Mohammed S Kamara anajiandaa kwa mechi ya mtaani ya soka katika kiwanja hiki kilicho nyuma ya kituo cha wazima moto. Mazoezi haya ni muhimu sana kwa kazi yake.
 • Santigi Bangura anazima moto ulizozuka kutokana na tatizo la umeme mjini Freetown na kusababisha kifo cha mwanamume mmoja.
 • Kikosi cha wazima moto wakati mwingine kukabiliwa na matusi kutoka kwa wenyeji wanapowasili kuchelewa. Hapa walitukanwa na hata kufukuzwa na hivyo kwenda bila ya hata kuzima moto
 • Mulk Sulaiman amekaa nje ya nyumba yake baada ya kufuzu katika kituo cha mafunzo kwa wazima moto. Tangu utotoni amekuwa akitaka kujiunga na kikosi cha wazima moto.
 • Naye bwana Maliki S Kamara alijiunga na kikosi hicho mwaka 1975 na alisifika sana kama afisaa mwenye nguvu zaidi kati ya wazima moto wote mjini Freetown

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.