Chakula kinavyoharibikia sokoni Afrika

19 Juni 2013 Imebadilishwa mwisho saa 09:34 GMT

Je unafahamu kiwango cha chakula kinachoharibikia sokoni ambacho kinachangia njaa Afrika? Picha na Emmanuel Igunza
Msanii na mwimbaji mashuhuri nchini Kenya Emmy Kosgei aligeuka muuza nyanya katika soko mashuhuri la mboga na matunda Nairobi, Marikiti
Hii ni Dhania ambayo imeharibika ikiwa sokoni. UNEP linasema kuwa thuluthi moja ya chakula Afrika hukaribika kabla ya hata kufika sokoni
Soko la Marikiti ndilo lenye idadi kubwa ya wauzaji wa mgoga na matunda. Chakula huletwa katika soko hili kutoka kote nchini Kenya
Shirika la UNEP liliamua kuhamasisha wauzaji wa sokoni juu ya kuhakikisha kuwa chakuka hakiharibika sokoni
Pamoja na kuwa ni hasara kwa wafanyabiashara kwa mazao yao kuharibikia sokoni, ni vibaya kwa chakula kuharibika wakati watu wengi wanakosa lishe bora duniani
Ann Mc'Creath ni mmiliki wa kampuni ya Kiko Romeo yenye kutengeza mitindo ya kisasa nchini Kenya, naye aligeuka na kuuza mboga katika soko la marikiti kwa siku hiyo
Wanafunzi wa shule ya upili ya St Georges nao pia walifika kwenye soko la Marikiti kujionea shughuli za uuzaji na hata kuwa wauzaji kwa siku hiyo
Machungwa yaliyoharibika wakati watoto wengi wanhitaji madini ya vitamin C . Hebu tafakari hilo!
Mwimbaji mashuhuri wa kanda ya Afrika Masharikji Amani alipokea maelezo kuhusu biashara kutoka kwa mama huyu
Kauli mbiu kwa wauzaji kuhakikisha kuwa uharibifu wa chakula hautokei katika soko lao
Biashara inaendelea kama kawaida