BBC navigation

Vifo vya majeshi ya A. Kusini.Kulikoni?

Imebadilishwa: 8 Aprili, 2013 - Saa 08:34 GMT

Media Player

Wiki jana wanajeshi 13 wa Afrika Kusini waliouawa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati walizikwa. Lakini kwa nini walikuwepo huko?

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Wiki jana wanajeshi 13 wa Afrika Kusini waliouawa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati walizikwa. Kulikuwa na madai kuwa wanajeshi hao walikuwa nchini humo kinyume na sheria na kulinda tu maslahi ya kibiashara ya chama tawala ANC.

Jarida moja la nchini humo lilidai kuwa baadhi ya washika dau katika chama cha ANC , wana mikataba ya kifahari na nchi hiyo huku na wao wakiwapa ulinzi kutoka kwa jeshi lao.

Lakini Rais Jacob Zuma alikanusha madai hayo na kusema kuwa ni kama matusi kwa mashujaa wa nchi hiyo.

Hata hivyo swali ambalo limekuwa likihojiwa ni kwa nini walikuwepo huko na hata wakakutwa na mauti? Omar Mutasa alimuhoji Bregedia Jenerali Qolani Mabanga ambaye ni msemaji wa jeshi la Afrika Kusini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.