BBC navigation

Angelina Jolie na kilio cha ubakaji DRC

Imebadilishwa: 29 Machi, 2013 - Saa 10:46 GMT

Media Player

Angela Jolie asema kuwa dunia nzima inapaswa kushughulikia tatizo la watu kutumia ubakaji kama silaha ya vita.

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

MuIgizaji wa Hollywood Angelina Jolie na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza,William Hague wameshirikiana katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuhamasisha kuhusu ubakaji.

Wawili hao walitembelea kambi moja mjini Goma ya wanawake waathiriwa wa ubakaji ili kuhamasisha kuhusu ubakaji katika maeneo ya vita.

Bwana Hague alisema kuwa tatizo la dhulma za kingono sharti lishughulikiwe ikiwa tunataka kumaliza tatizo la vita. Angelina Jolie ambaye ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa alisema kuwa dunia nzima inapaswa kushughulikia tatizo la watu kutumia ubakaji kama silaha ya vita.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.