BBC navigation

Damu yamwagika Tana

Imebadilishwa: 21 Septemba, 2012 - Saa 14:48 GMT

Media Player

Damu yamwagika Tana River baada ya zaidi ya watu 100 kuuawa katika mapigano kati ya wapokomo na waorma. Ni nini kilichojiri?

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Polisi na wataalamu wa uchunguzi wa maiti walipigwa na butwaa baada ya kukosa kupata chochote katika kilichodhaniwa kuwa makaburi ya siri katika eneo la Tana River kufuatia wiwki tatu za makabiliano kati ya jamii mbili hasimu.

Mzozo wa kikabila kati ya wapokomo na waorma ambao ulisababisha mauaji ya zaidi ya watu miamoja ndio umeanza kutulia. Maelfu ya watu waliachwa bila makao huku nyumba zikiteketezwa.

Taarifa za awali zilisema kuwa huenda watu wa jamii ya wapokomo iliwaondoa maiti katika makaburi hayo wakati polisi walipokuwa wanasubiri kibali cha mahakama kuweza kuyafukua. Sasa hali ilikuwa vipi katika eneo hilo na nini hasa chanzo za mzozo huu? Taarifa hii inasimulia zaidi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.