bbc.co.uk navigation

Nigeria mpira wa mitaani

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2011 - Saa 15:34 GMT

Kandanda la mitaani dhidi ya kutoaminiana

  • Soka la mitaani nchini Nigeria
    Kandanda mara nyingi huitwa mchezo wa watu. Hii ni kweli kabisa nchini Nigeria ambapo katika ngazi za chini kuhamasisha na kuunganisha jamii masikini. Picha na maelezo: Nseabasi Akpan
  • Kandanda la mitaani Nigeria
    Ibadan, katika jimbo la Oyo nchini Nigeria, ni moja la miji mikubwa Afrika Magharibi, ikiwa na idadi ya watu wapataa karibu milioni tatu. Jiji hili limeshuhudia kuzuka kwa ghasia kabla na wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2011.
  • Kandanda la mitaani Nigeria
    Ibadan pia ni mahala pa watu kukutana na makundi mbalimbali bila kujali dini, utamaduni au siasa, kutokana na mapenzi ya soka.
  • Kandanda la mitaani Nigeria
    Kila asubuhi na jioni vijana wa Ibadan hujipanga na kujigawanya katika timu na kuvaa sare mbalimbali na viatu pia, na kwenda uwanjani, au mitaani, au eneo lolote la wazi 'kusakata gozi'.
  • Kandanda la mitaani Nigeria
    Wakati mwingine timu hujigawanya kutokana na mitaa wanayoishi. wakati mwingine, umri ndio unaamua nani acheze na nani - kwa kutazama zaidi urefu wa wachezaji, na sio tarehe za kuzaliwa.
  • Kandanda la mitaani Nigeria
    Lengo lao ni moja: Kuweza siku moja kubutia timu kubwa za soka ambazo zinalipa fedha nyingi, nyumbani au hata nje ya nchi, ili kuyafanya maisha yao na familia zao kuwa bora zaidi.
  • Kandanda la mitaani Nigeria
    Akeeb Kareem, mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Sango, mjini Ibadan anasema kandanda la mitaani ni muhimu katika kuhakikisha vijana wa jiji hilo wanakuwa na shughuli ya kufanya.
  • Kandanda la mitaani Nigeria
    Mtazamo wake ni kuwa iwapo serikali inataka kupata tena medali ya dhahabu katika soka kama ilivyokuwa miaka 15 iliyopita nchini Marekani, kinachohitajika kufanyika ni kutazama mitaa ya Nigeria ambapo vijana wanacheza kwa ari wakiwa na ndoto ya siku moja kuwa nyota wa Nigeria.

Mpira wa miguumara nyingi imekuwakuitwamchezowatu.Hiini kwelikatikaNigeriaambapokatika ngazi za chininikuwahamasishanaunaunganishajamiimaskini

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.