Mjadala wa Kaunti ya Kajiado

24 Novemba 2013 Imebadilishwa mwisho saa 13:04 GMT

Walioshiriki katika mjadala wa kaunti ya Kajiado.
Wenyeji wa Kajiado wanaona kwamba kaunti yao ni tajiri, ilhali rasilimali inatumika viibaya.
Wananchi wanasema hawapati manufaa ya rasilimai kama uzalishaji wa simiti na magadi, na mbuga za wanyama.
Utajiri wa kaunti una maanisha utajiri wa wenyeji wa kaunti? Wakaazi wa Kajiado walitaka kujua ni vipi haswa utajiri utawafikia.
Au manufaa ya ugatuzi yanachelewa kufikia Kajiado kwa sababu ya mvutano ulio kati ya viongozi wa kaunti hii?
Maswali haya yalijadiliwa kwa kina katika kipindi hiki.