|
|
 |
 |
 |
Mahojiano na Rais Kabila

Rais Kabila ahojiwa na Tido Mhando, Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC
|
Sikiliza mahojiano ya pekee
Kabila akubali kuhojiwa
Marehemu Rais Laurent Desire Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, aliuwawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake siku chache zilizopita. Wakati wa uhai wake, kiongozi huyu, aliyetawala kwa kipindi kifupi cha chini ya miaka minne, hakupendelea sana kufanya mahojiano ya ana kwa ana na waandishi wa habari, na hasa tangu kuanza kwa mapigano yanayoendelea nchini humo hivi sasa.
Lakini, kiasi cha kama mwezi mmoja tu kabla ya kufariki kwake, hayati Kabila, alikubali kufanya mahojiano ya kina na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Tido Mhando, huko mjini
Mobutu, Rwanda na Uganda
Katika mahojiano hayo, yaliyofanyika kwenye makao makuu ya Rais Kabila (Palais de Marbre), mahali ambapo ndipo alipouawa, marehemu aliweza kuzungumzia maisha yake wakati wa harakati za kutaka kuung'oa utawala wa kiongozi aliyemtangulia, marehemu Mobutu.
Pia alielezea kwa kirefu jinsi hatimaye, kwa msaada wa majeshi ya Rwanda alivyofanikiwa kutwaa madaraka na sababu zilizopelekea kuzuka kwa mgogoro baina yake na Rwanda, Uganda na Burundi.
Ya kwanza na ya mwisho
Vile vile, kwenye mahojiano haya ambayo, yalitangazwa na Idhaa ya kiswahili ya BBC hapo Desemba 28, 2000, hayati Kabila anajibu shutuma mbambali zilizoikabili serikali yake na yeye binafsi. Sasa kwenye ukurasa huu, unaweza kuyasikiliza tena mahojiano hayo, ya kwanza kabisa kwa kipindi cha miaka mitatu na ya mwisho, baina ya Tido Mhando na Rais Laurent Kabila.
|
|
 |
 |
|
|
 |
 |
 |
 |
 |
|
|
| BBC haina dhamana juu ya yale yaliyoandikwa katika kurasa za internet za mashirika mengine |
 |
| Wasiliana Nasi |
 |
| Email:swahili@bbc.co.uk |
 |
Au tuandikie Bush House, Strand, London WC2B 4PH |
Tel: + 44 207 557 2502 Fax: + 44 207 240 4637
|
|