|
Kimasomaso
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Mbona vijana wanaendelea kujihusisha na ngono isio salama licha ya juhudi kubwa za uhamasishaji ambazo zimefanywa?
Kulingana na utafiti uliofanywa nchini Kenya miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu, takriban asilimia 77 ya wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Nairobi washapima hali yao ya HIV. Utafiti huo uliyofanywa hivi majuzi na shirika la ‘I Choose Life’ kuwa licha ya asilimia hiyo kubwa ya wanafunzi kujua hali yao ya virusi, takriban asilimia 64 ya wanafunzi hao bado wanajihusisha na ngono bila kutumia kinga, huku asilimia 8 ya wanafunzi wakisema kwamba hawatumii kinga yoyote. Asilimia 47 ya wanafunzi hao walisema ya kwamba hawatambui hatari zilizopo wanapojihusisha na ngono bila kutumia kinga. Utafiti huu unaonyesha kuwa kati ya wale wanaoshiriki ngono bila kutumia kinga ni asilimia kubwa ya wale waliopima tayari hali yao ya virusi. Inashangaza kuwa wanafunzi wa chuo kikuu wanaotarajiwa kuwa wepesi wa kuelewa na walio na habari zaidi juu ya hatari husika, ndio mwanzo wanaojitosa kifudikifudi katika uraibu huu wa ngono ya kiholela. Hili ni jambo linalowaweka katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya ukimwi, magonjwa ya zinaa na hata wasichana kupata mimba wasiotarajia. Licha ya chuo kikuu cha Nairobi kufanya somo la ‘HIV AIDS’ kuwa somo la lazima hivi maajuzi na serikali ya Kenya kujizatiti kupunguza idadi ya vijana wa vyuo vikuu wanaoshiriki katika ngono ya mapema na isiyo salama, ukweli ni kwamba vijana wengi bado wanajiweka katika tabia hizi zinazohatarisha afya yao. Swali ni je, nini kingine kifanywe ili kuwaepusha vijana na janga la ukimwi na hatari nyingine zinazotokana na ngono isio salama? Tunazungumza na baadhi ya wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, tunaongea pia na Mkuu wa NASCOP-Shirika la kudhibiti ukimwi nchini pamoja na mkuu wa maswala ya afya ya wanafunzi katika chuo kikuu cha Nairobi. Tuandikie kupitia mtandao wa facebook, group yetu ni “KIMASOMASO”. Au kupitia e-mail: kimasomaso@bbc.co.uk au unaweza kututumia ujumbe mfupi kwa nambari hii +447786202005, unaweza pia kututumia barua kwa sanduku la posta 58621, Nairobi Kenya
|
VIUNGO VYA MTANDAO WA HAPA HAPA
Kuhusu Kimasomaso29 Januari, 2009 | Vivutio
Shughuli za Kimasomaso29 Januari, 2009 | Vivutio
Masimulizi ya washiriki06 Januari, 2009 | Vivutio
Ukweli wa mambo29 Januari, 2009 | Vivutio
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||