BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 09 Novemba, 2009 - Imetolewa 16:06 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Mafuriko yakwamisha magari Kenya
 
Baada ya ukame wa muda mrefu, mvua kubwa zilipoanza kunyesha katika mkoa wa Kaskazini Mashariki nchini Kenya zilisababisha mafuriko yaliyobomoa miundo mbinu kama barabara. Mwandishi wetu Bashkash Jugsoday alishuhudia uharibifu huo, zifuatazo ni baadhi ya picha alizopiga katika barabara ya Dabaab kwenda Garissa.

Magari ya mizigo zaidi ya 40 yakiwa yamebeba chakula cha misaada ya wakimbizi wa kisomali yalikwama kutokana na barabara kuwa hazipitiki.

Kutokana na barabara kuwa za vumbi, mvua imefanya zijae tope. Zaidi ya wakimbizi 270,000 wa kisomali walioko katika kambi tatu hutegemea chakula kinachopelekwa kwa njia ya barabara kila baada ya siku 15.

Inahofiwa kuwa endapo hali hiyo itaendelea, wakimbizi hao watakabiliwa na shida kubwa ya chakula. Barabara nyingine zilizoathirika ni zile za Garissa, Wajir-Mandera, Wajir na Garissa kwenda Mombasa.

Kwa kawaida malori hayo husafirisha shehena ya chakula kutoka Mombasa kwenda Dabaad yapata kilometa 630. Tayari kuna taarifa ya kupungua kwa mahitaji muhimu kama sukari, mchele, na mafuta ya kupikia.

Madereva na wasaidizi wao wamekwama katika barabara hizo kwa kipindi cha zaidi ya siku 10, wakilalamika kuwa hawana chakula wala maji.


 
 
VIUNGO VYA MTANDAO WA HAPA HAPA
Ukame waiathiri Kenya
16 Oktoba, 2009 | Vivutio
Mwana wa Mohammed Ali akiwa Kinshasa
02 Novemba, 2009 | Vivutio
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha