BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 16 Oktoba, 2009 - Imetolewa 10:35 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Ukame waiathiri Kenya
 
Hivi karibuni mwandishi wetu Bashkas Jugsoday alizuru sehemu kadhaa za mkoa wa Kakazini Mashariki nchini Kenya ambako ukame umeathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya wakazi na mifugo yako. Haya ndiyo uliyoshuhudia katika safari yake.....

Mifugo ya kila aina inaangamia kutokana na ukosefu wa maji na chakula...ni ukame mkali.

Mfugaji akimvuta ng'ombe ambaye uhai wake umekatizwa na ukame, kwa nyuma unaweza kuona mbuzi kadhaa wamekufa.

Punda yu hoi bin taaban, kazi ngumu na ukame vinakwaza maisha yake. Mkazi huyu anajaribu kumsaidia punda wake kusimama.

Ngamia, wanyama wanaojulikana kwa ustahimilivu wao jangwani, ndiyo tegemeo kwa baadhi ya wakazi kuchota maji.

Wanyama na binadamu wanagombea maji, hili ni eneo la kunyweshea wanyama kando na sehemu ya kuchotea maji kwa matumizi ya binadamu.

Wenye uwezo husubiri maji majumbani ambako gari kama hili huyafikisha na kuwauzia.

Visima vya kila aina vimechimbwa, mkazi huyo akikwangua maji kutoka kisimani, japo si mengi yanapatikana.


 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha