Skip to main contentAccess keys helpA-Z index
BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 26 Juni, 2009 - Imetolewa 11:35 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Maoni: Michael Jackson
 
Yafuatayo ni baadhi ya maoni yaliyotumwa na watu mbali mbali kuhusu kifo cha mwanamuziki Michael Jackson, aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 50.

Namuombea kila la kheri huko anakokwenda pumzika kwa mengi aliyofanya hapa dunia. Nilisikitishwa kusikia habari yake ya kifo chake jana usiku wa saa tano saa za hapa UK. Mola amuweke mahali pema nimecheza muziki wake enzi bad na mingine mingi na kuvaa jeans zake xmas and edd-fitr.
Noel Miron - Chelmsford, United Kingdom

Tutamkumbuka kwa msaada mkubwa aliutoa yeye na wanamuziki wenzake. Waliimba wimbo wa we are the world, we are the one, pesa ziliisha wenye njaa kule Ethiopia. Huo ni mchango mkubwa sana. Ni fundisho kwa wanamuziki wote.
Goodluck Msenga - Dar Es Salaam, Tanzania

Michael atakumbukwa kwa mengi hususani moyo wake wa kupenda watoto, ila aliniudhi alipokuwa anaukana Uafrika wake, nawasihi wasanii wengine waige mazuri wala si mabaya kama kujibadili n.k. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amina.
Aurelia Mushi - Dodoma, Tanzania

Michael Jackson, alikuwa mwafrika aliyeuasi Uafrika. Kitendo cha kuikana rangi na haiba yake ya Kiafrika, hakika ilikuwa ni dharau kubwa sana kwa watu wote weusi duniani. Wazungu walimpenda kwa sababu alijitahidi kuonekana kama wao. Mwisho wa siku akashindwa.

Tunaweza kusema mengi kuhusu kifo chake, lakini kilicho wazi ni kwamba kemikali alizotumia kuukana Uafrika wake, zimegharimu. Hili ni somo kwa wengine wa aina hiyo, hasa ndugu zetu wa Afrika ya Kati ambao wanaona kuimba wakiwa na sura na rangi ya kiafrika, ni makosa!!!

Michael amefariki. Ni jambo la kusikitisha. nitamkumbuka si kwa nyimbo na majonjo yake jukwaani, bali kwa kuwa muasi halisi wa asili yake. Tukumbuke kuwa hakuna binadamu anayeweza kumhariri Mungu!!!
Manyerere Jackton - Dar Es Salaam, Tanzania

Kwakweli tutabaki tunamkumbuka daima milele, Michael Jackson isitoshe yeye mwenyewe alitabiri mapema kifo chake isikuchanganye sana kwasababu kifo kipo nakitaendelea kuwepo kwasababu sisi sote niwasafiri tumekujakutembeya apa duniani tupo njiani kuelekea uko unakoenda, tumuombe yetu mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu maalipema peponi, Amena.
Rizo Babingwa - Aalborg, Danmark

Hakika ulimwengu umempoteza mtu muhimu sana namkumbuka katika staili yake ya uchezaji na uimbaji hakika pengo lake halita zibika. Hatutakusahau milele daima.
Benny Wissa - Mbeya, Tanzania

Miaka ya themanini (1980's) kulikuwa na mavazi ya (Jacksons 5 cadet) na haswa watoto ndiyo walizipenda sana. Kama wazazi hawajanunua hizo nguo kwa ajili ya krismasi, basi nyumbani hapakaliki. Zilikuwa zinagharimu shillingi 5000 za kitanzania.
Richard Kweka - Dubbo, Australia

Namtakia kila la heri anapokwenda.
Haririmana Francois - San Antonio, Marekani

Michael alikuwa mwanamuziki hodari sana naitakia familia yake faraja kubwa sana kipindi hiki kigumu kwao.
Gilbert Kessy - Dar Es Salaam, Tanzania

Nawashukuru pole wapenzi wa popo kwa msiba wa Jackson.
Faraja Chinyuka - Arusha, Tanzania

Hakika hakuna atakayebakia duniani, Michael Jackson unatangulia tu. Mungu akulaze pema.
Hakim Kombo - Nungwi, Tanzania

Nilishtuka kidogo niliposikia taarifa juu ya kifo cha Michael Jackson. Nitamkumbuka sana katika juhudi zake za kuchangia watu mbalimbali wanaoteseka hapa Afrika kwa kutumia kipaji chake cha muziki,mfano wimbo wa Heal the World na US For Africa, ziliweza kuchangisha fedha kwa ajili ya Africa. Mungu aitie moyo familia yake hasa kipindi hiki kigumu cha msiba wake.
Robert Kiondo - Moshi, Tanzania

Nawapa pole sana wanamuziki na mashabiki wake na dunia kwa ujumla baada ya kifo cha mwana muziki Michael Jackson kufariki dunia, alikuwa Pele akaja Maradonna akaja Zidane kufa yeye kusiwe ndio mwisho wa muziki wa pop atakuja Akon na wenginewe. Mungu ailaze pema roho yake.
Mohammed Mshangama - Dar Es Salaam, Tanzania

Kila kitu kina mwanzo na mwisho na huu ndio mwisho wake Michael Jackson tumuombee dua mungu ampumzishe pahala pema "Ameen".
Khamis Foum - Bububu, Zanzibar

Mimi kitu ninacho kumbuka ni kwamba kijana huyu aliyefariki dunia alikuwa shujaa, kwa sababu ni kijana aliyekuwa kafanikiwa kimaisha kwa ajili ya jasho lake haitoshi kazaliwa katika familia dunia, pamoja na kashfa nyingi tu zilizomkumba alikuwa bado ni kipenzi cha watu.
Lanky Bahama - Kalsdonk, Uholanzi

Mungu amlaze pema Michael Jackson.Tukiachana na mimi Wako Jacko atakumbukwa na dunia nzima. Nachokumbuka toka Jacko ni jinsi alivyokuwa akicheza, hivyo kaka yangu alikuwa ananivisha kama Jacko ili nicheze, hakika si mimi tu ambaye nilikuwa nauiga mtindo huo wa marehemu Jackson bali wengi tu,haswa huku Tanzania.

Kusema kweli ni pengo kubwa aliloacha. Nakumbuka mengi tu kuhusu Jacko wakati nilipopewa zawadi shuleni nilivyoucheza wimbo wake unaokwenda kwa jina la 'You Rock Ma World'. Pia sisahau kamwe nilivyokuwa namwaga machozi wakati Jacko alivyofikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya ulawiti. Buriani Michael Jackson.
Ali Jumanne Ramadhani - Arusha, Tanzania

Kifo cha Michael Jackson kimetugusa wengi hususan sisi mashabiki wa pop, mimi binafsi nakikumbuka kibao chake cha "Thriller", akinengua stejini kwa staili ya vidole huwa nakumbuka mbali sana. Tumuenzi kwa yale mema aliyoyatenda na tumuombe katika safari yake ya mbinguni. Mungu amlaze mahali pema peponi Amina.
Charles Makange - Tanga, Tanzania

Mimi nilikuwa nataka kujua je Michael Jackson kafa akiwa muislam? Kwasababu nilisikia kasilimu. Maoni zaidi BBC inatusaidia sana hasa sisi wanafunzi hongereni kwa hilo.
Ashraff al-Kalbany - Zanzibar

Michel Jackson lala salama na uanze maisha mapya kaburini.
Said Mihala - Stone Town, Zanzibar

Nimepokea kwa masikitiko sana kifo cha Wacko Jacko.Ulimwengu wa muziki umempoteza mtu ambaye itakuwa ngumu kuziba pengo lake.Tutamkumbuka Michael Jackson daima, apumzike kwa amani.
Stephen Bahati - Serengeti, Tanzania

Michael Jackson tulimpenda sana kwa kweli tumepoteza mtu muhimu katika ulimwengu wa pop, sijaona kama Michael na wanamuziki wanalijua hilo. Maoni yangu tumuenzi kwa hali na mali kwa yote aliyoyafanya katika uhai wake kama vile kusaidia watoto yatima na kupinga unyanyasaji wa haina yoyote duniani.
Edwin Bajwauka - Dar Es Salaam, Tanzania

Nimehuzunishwa sana na kifo cha aliyekuwa gwiji wa muziki wa pop duniani. Ni kweli hiki ni kipindi kigumu sana kwa familia ya Jacko pamoja na mashabiki wake. Tunafahamu na kutambua mchango wake katika harakati za watu weusi.
Ibrahim Ramadhani - Dar Es Salaam, Tanzania

Ni tabia yake ya kuukana uafrika na dharau iliyopindukia ndiyo mambo ambayo daima atakumbukwa kwa hayo, ukiacha hayo ni mwanamuziki aliyekuwa wa viwango vya juu kabisa aliyepata kuishi katika karne ya 20.Jina la Bwana lihimidiwe.
Zebedayo Msigala - Dodoma, Tanzania

Tunasitika nasikitika kumpoteza Michael Jackson tutamkumbuka kumpoteza Michael Jackson tutamkumbuka uchezaji wake mahiri wa muziki wa pop.
Matiku Matiku - Dar Es Salaam, Tanzania

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha