|
Michael Jackson
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Hizi ni baadhi tu ya picha zinazotukumbusha maisha ya mwanamuziki Michael Jackson aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 50.
Michael Jackson alianza shughuli za muziki akiwa na kaka zake wakiunda kundi la Jackson 5, na kundi hilo lilipofyatua kibao chao cha kwanza "I Want You Back" mwaka 1969, kiligonga namba moja kwa umaarufu - wakati Michael alikuwa na umri wa miaka 11 tu.
Baada ya hapo Michael alijitenga na kaka zake kisha akapakua kibao "Off the Wall" mwaka 1978, lakini Thriller iliyotolewa miaka minne baadaye ndiyo ilifanya muziki wa pop kupata umaarufu mpya, ilifanikiwa kuuza nakala milioni 65.
Michael aliipua "Bad" mwaka 1987 na baada ya hapo kufanya ziara ya matamasha ya kwanza duniani, nchini Uingereza tiketi katika uwanja wa Wembley ziliuzwa zote alipofanya matamasha saba na kuweka rekodi ya mashabiki.
Katika maisha yake Michael alizongwa na utata kila alikoenda. Mwaka 1994 alimwoa Lisa Marie Presley baada ya kuwa wamekutana kwa mara ya kwanza mwaka 1975. Walitalikiana chini ya miaka miwili baadaye.
Mwaka 2003 kibali kilitolewa kukamatwa kwa Michael akikabiliwa na mashtaka ya kunajisi mtoto mwenye umri wa miaka 14. Baada ya kesi iliyoungura kwa miezi mitano na kumalizika 2005, mwanamuziki huyo hakupatikana na hatia yoyote.
Michael alihama kutoka makazi yake ya Neverland na alienda kuishi Dubai. Sherehe yake ya kutimiza miaka 50 ilifanyika Las Vegas. Amekuwa akionekana kuwa na afya dhaifu, ingawa alikuwa akijiandaa kufanya mfululizo wa matamasha jijini London. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||