Skip to main contentAccess keys helpA-Z index
BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 29 Januari, 2009 - Imetolewa 14:49 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Shughuli za Kimasomaso
 
Kama ilivyokuwa katika awamu ya kwanza, Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilitoa vipindi kila wiki, iliyojumuisha simulizi na majadiliano, na kupeperushwa hewani kwa takriban wasikilizaji milioni 10 katika Afrika ya Mashariki.

Utafiti unaonyesha kwamba idadi hii iliongezeka kwa ajili ya kipindi cha Kimasomaso kwenda hewani na sasa inafikia millioni 16.

Tom Japanni ambaye mwanzoni mwa kipindi hiki katika msimu wa kwanza alikuwa mtayarishaji msaidizi na mtangazaji mwenza, ndiye sasa mtayarishaji mkuu wa kipindi.

Baadhi ya washiriki wa Kimasomaso katika picha ya pamoja jijini Nairobi.

Tom ambaye amefanya kazi katika vipindi vya vijana kwa muda wa miaka mitano iliyopita katika taaluma ya uanahabari, alikuwa akisaidiana kutangaza kipindi na Salome Nduku ambaye alikuwa mwanafunzi wa taaluma ya udaktari katika chuo kikuu cha Nairobi.

Kwa muda mrefu sasa, Amina Abubakar ndiye naibu mtayarishaji na mtangazaji mwenza wa kipindi cha Kimasomaso.

Mtayarishi wa kipindi Tom Japanni na Naibu wake Amina Abubakar

Kimasomaso kinatayarishwa kila wiki na kikundi cha watu watatu – chini ya usimamizi wa Mkurugenzi kuu wa BBC World Service Trust, Joerg Stalhut pamoja na Mhariri Mkuu wa ofisi ya BBC Nairobi na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akiwa London.

Katika kiwango cha maandalizi, watayarishaji kila mara huwa waangalifu kwa kujadili na kubadilishana maoni yao chini ya uongozi kutoka kwa msimamizi wa mradi akiwa London.

Jambo lingine la muhimu ni kuhakikisha ujumbe unaotolewa katika vipindi ni sanifu na kweli, na usiopendela au kumtuhumu mtu yeyote. Watayarishaji wanahakikisha kuwa kipindi hakiwadhalilishi wala kuhubiriwa vijana.

Msimamo muhimu wa Kimasomaso ni kuwawezesha vijana kufanya uamuzi wao binafsi kuhusu tabia zao baada ya kupokea ujumbe sanifu na madhubuti kuhusu jinsia na afya ya uzazi, pamoja na haki walizo nazo kisheria. Kando na kazi ya utayarishaji na utangazaji wa kipindi inayofanywa na Tom Japanni na Amina Abubakar, kunae pia Sam Otieno anaeshughulikia utafiti na mtandao pamoja na Veronica Gachienge anashughulikia maswala ya uhasibu.

Veronica Gachienge, Sam Otieno, Amina Abubakar (kusimama) na Tom Japanni (kakaa)

Kwa vile idhaa ya Kiswahili ya BBC hutangazia eneo zima linalozungumza Kiswahili katika afrika ya mashariki, ni muhimu kusikiliza michango kutoka sehemu zote katika eneo hili - Tanzania, Kenya, Uganda, DRC, Rwanda na Burundi, sehemu za mashambani vilevile miji na majiji.

Kipindi hupeperushwa mara tatu kwa wiki ( Jumamosi jioni saa 12 na Jumapili asubuhi (saa 12) na jioni (saa moja unusu) unaweza pia kusikiliza kupitia tovuti katika BBCSwahili.com.

 
 
VIUNGO VYA MTANDAO WA HAPA HAPA
Kuhusu Kimasomaso
29 Januari, 2009 | Vivutio
Masimulizi ya washiriki
06 Januari, 2009 | Vivutio
Ukweli wa mambo
29 Januari, 2009 | Vivutio
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha