|
Kuhusu Kimasomaso
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Kipindi cha Kimasomaso kilitokana na mradi wa pamoja kati ya BBC na shirika la IPPF (International Planned Parenthood Federation)
uliojulikana kama Sexwise.
Mradi huo wa Sexwise ulitoa habari kuhusu afya ya uzazi na afya bora ya watu binafsi pamoja na kuwapa njia tofauti za kufanya maamuzi na kuwajulisha haki zao.
Katika mradi huu, wanaharakati wengi kutoka sekta ya maswala ya afya ya uzazi mashinani walihusishwa.Afrika Mashariki, kwa mfano, ilikuwa jambo la kuvutia kukutana na vijana wakifanya kazi kama waelimishaji rika katika kituo cha vijana cha Eastleigh, jijini Nairobi. Waelimishaji rika hawa vijana, walihisi kwamba ukosefu wa elimu kuhusiana na mambo ya kijinsia pamoja na dhana husika ndiyo iliyokuwa changamoto kubwa inayofaa kukabiliwa. Kwa maoni yao, maswala muhimu zaidi yanayowahusu vijana katika Afrika Mashariki, hasa katika nyanja ya afya ya uzazi, ni ukosefu wa elimu madhubuti kuhusu afya ya uzazi, ukosefu wa ujasiri na uzoefu katika kujadili na kufanya uamuzi kuhusu mahusiano na kuelewa jinsia zao, magonjwa ya zinaa, mimba za mapema na uavyaji mimba au abortion. Umuhimu wa Kimasomaso
Kutokana na Sexwise, iligundualiwa kwamba kuna shinikizo kubwa la kutaka kukandamiza mijadala huru kuhusu maswala ya ngono na afya ya uzazi katika eneo hili. Takwimu za afya ya umma kuhusu UKIMWI, ndoa za mapema na utoaji mimba usio salama zinajieleza kikamilifu; hadithi kuhusu matukio ambayo hayangetokea iwapo watu wangekuwa na ufahamu sahihi na uhuru wa kuchukua maamuzi yao wenyewe. Ili kupiga hatua yoyote muhimu, ni lazima kufahamu na kukubali kwamba swala la afya ya uzazi siyo tu swala la kiafya pekee. Kwa kiasi kikubwa ni kuhusu umaskini, ukosefu wa usawa wa kijinsia na mila, na ni mkusanyiko wa maswala haya kunakochangia uelewa wa watu kuhusu ujinsia wao, ambayo kwa wengi ni mwiko. Katika tajiriba yetu, upendo mkubwa na imani inayohusishwa na usikilizaji wa redio unaweza kutumiwa kutoa jukwaa mahsusi la kujadili kwa undani maswala nyeti na mazito yanyayohusiana na afya ya uzazi.
|
VIUNGO VYA MTANDAO WA HAPA HAPA
Shughuli za Kimasomaso29 Januari, 2009 | Vivutio
Masimulizi ya washiriki06 Januari, 2009 | Vivutio
Ukweli wa mambo29 Januari, 2009 | Vivutio
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||