BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 24 Agosti, 2008 - Imetolewa 19:02 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Tukumbuke wenzetu
 

Balozi wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Bw Zakary Muburi Mwita akizungumza mbele ya wageni waliofika nyumbani kwake kukumbuka watu waliouawa kwenye mashambulio ya mabomu balozi za Marekani Nairobi na Dar Es Salaam Agosti 1998.Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilirusha matangazo moja kwa moja kutoka New York.

Anna Mwalago akisoma shairi katika siku ya kumbu kumbu hiyo kwenye makazi ya balozi wa Kenya huko Umoja wa Mataifa mjini New York.

Abbas Byabusha ambaye mkewe aliathirika kwa mashambulio ya Septemba 11 akiwa na Stanley Mutuma, mwanafunzi wa sheria nchini Kenya ambaye alipofuka macho wakati wa mashambulio hayo na mtangazaji wa BBC, Mariam Omar mjini New York siku ya kumbu kumbu.

Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Mariam Omar akiwa maeneo ya Manhattan wakati akiwa Marekani kwa kumbu kumbu za miaka 10 ya mashambulio ya mabomu Afrika Mashariki.

Caroline Wavai akizungumza mbele ya wageni waliokusanyika nyumbani kwa Bw Zakary Muburi Mwita [aliyesimama nyuma].

Bendi ya muziki ya Jabali ikitumbuiza

Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini matangazo ya Dira ya Dunia yaliyoruishwa moja kwa moja kutoka New York, tarehe 7 mwezi Agosti 2008.


 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha