BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 07 Agosti, 2008 - Imetolewa 14:25 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Kumbu kumbu ya miaka 10
 
Fuatilia ziara yao huko Marekani - Mariam Omar mtangazaji wa BBC akiwa na Stanley Mutuma, raia wa Kenya alipofuka kutokana na mashambulio ya mabomu kwenye balozi za Marekani huko Kenya na Tanzania.Walizuru Marekani kama sehemu ya kumbu kumbu ya miaka 10 tangu kutokea kwa mashambulio hayo.

Msimamizi wa matangazo wa BBC, Mariam Omar akiwa na Stanley Mutama raia wa Kenya anayeshiriki katika vipindi maalum vya Idhaa ya Kiswahili ya BBC kama kumbu kumbu ya miaka 10 tangu kutokea kwa mashambulio ya mabomu kwenye balozi za Marekani huko Tanzania na Kenya.Hapa walikuwa Boston katika mazungumzo na ndugu wa watu waliopoteza maisha katika mashambulio ya mabomu ya New York na Washington.

Balozi wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Bw Zakary Muburi Mwita akizungumza mbele ya wageni waliofika nyumbani kwake kukumbuka watu waliouawa kwenye mashambulio ya mabomu balozi za Marekani Nairobi na Dar Es Salaam.

Stanley Mutuma akiwa na Balozi wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Bw Zakary Muita alipomtembelea ofisini kwake.

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Augustine Mahiga [mwenye tai], akiwa katika picha ya pamoja na Mariam Omar wa BBC na Stanley Mutama aliyenusurika mashambulio ya mabomu Nairobi mwaka 1998.

Mtangazaji wa BBC, Mariam Omar akiwa na Stanley Mutuma walipozuru viwanja vya Ground Zero, yalipokuwepo majengo ya Twin Towers jijini New York, hapa ndipo yalipotokea mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001.

Familia za waathirika wa mashambulio ya mabomu ya Septemba 11 wakiwa na Stanley Mutuma, aliyepofuka macho kutokana na mashambulio ya mabomu kwenye ubalozi wa Marekani jijini Nairobi.

Waliokaa pamoja kulia ni Mariam Omar mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC na Stanley Mutuma kijana aliyepoteza uwezo wa kuona kutokana na shambulio la mabomu kwenye ubalozi wa Marekani jijini Nairobi wametembelea sehemu mbali mbali za Marekani.Hapa wakiwa Boston katika shughuli iliyowakutanisha watu kutoka Afrika Mashariki wanaoishi nchini Marekani, walipokutana kumkaribisha kijana Stanley.


 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha