22 Juni, 2007 - Imetolewa 14:16 GMT
Hata mwaka 1955 jengo la Bush House, makao ya BBC World Service, lilikuwa ni eneo lenye shughuli nyingi sana kama inavyoonekana kwenye picha hii.Idhaa ya Kiswahili imekuwa hapa tangu mwaka 1957. Huyu ndiye hayati Oscar Kambona, mtangazaji aliyerusha matangazo ya kwanza ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC tarehe 27 mwezi Juni mwaka 1957. Alifariki Uingereza akiwa na umri wa miaka 68. Abdulaziz Yacoub wa Idhaa ya Kiswahili akistajabia gari aina ya Rolls Royce muundo wa Silver Cloud kwenye maonyesho ya magari jijini London mwaka 1958. Zeyana Seif mmoja wa watangazaji wa kwanza wa kike akiwa na wenzake mwaka 1959. Mtangazaji Hassan Mazoa wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akijiandaa kwa kipindi cha muziki enzi hizo. Mtangazaji Alois Ngosso wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akituma ripoti kutoka kwenye maonyesho ya kimataifa ya mashua kwa kipindi cha kila Jumamosi. David Wakati mmoja wa watangazaji wa kwanza ambaye baadaye alirejea nyumbani Tanzania na kuwa mkuu wa redio ya taifa- RTD. Watangazaji Athmani Magoma, Mohamed Salim Said Kwegyir Munthali na Hamza Kassongo wakiwa na Engela akiwaonyesha jinsi ya kutumia kinanda.






