BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 22 Juni, 2007 - Imetolewa 14:16 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe Chapisha
Katika picha: Historia yetu
 

Bush House, 1955.

Hata mwaka 1955 jengo la Bush House, makao ya BBC World Service, lilikuwa ni eneo lenye shughuli nyingi sana kama inavyoonekana kwenye picha hii.Idhaa ya Kiswahili imekuwa hapa tangu mwaka 1957.

Oscar Kambona, 1957.

Huyu ndiye hayati Oscar Kambona, mtangazaji aliyerusha matangazo ya kwanza ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC tarehe 27 mwezi Juni mwaka 1957. Alifariki Uingereza akiwa na umri wa miaka 68.

Abdul Aziz, 1958.

Abdulaziz Yacoub wa Idhaa ya Kiswahili akistajabia gari aina ya Rolls Royce muundo wa Silver Cloud kwenye maonyesho ya magari jijini London mwaka 1958.

BBC Swahili, 1959.

Zeyana Seif mmoja wa watangazaji wa kwanza wa kike akiwa na wenzake mwaka 1959.

Hassan Mazoa, BBC Swahili

Mtangazaji Hassan Mazoa wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akijiandaa kwa kipindi cha muziki enzi hizo.

Alois Ngosso, BBC Swahili

Mtangazaji Alois Ngosso wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akituma ripoti kutoka kwenye maonyesho ya kimataifa ya mashua kwa kipindi cha kila Jumamosi.

David Wakati, BBC Swahili

David Wakati mmoja wa watangazaji wa kwanza ambaye baadaye alirejea nyumbani Tanzania na kuwa mkuu wa redio ya taifa- RTD.

BBC Swahili

Watangazaji Athmani Magoma, Mohamed Salim Said Kwegyir Munthali na Hamza Kassongo wakiwa na Engela akiwaonyesha jinsi ya kutumia kinanda.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha