|
BBC Ulimwengu wa Soka
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Idhaa ya Kiswahili ya BBC ikishirikiana na redio washirika, siku ya Jumamosi, tarehe 18 mwezi Julai 2009, tutajadili ni kwa nini viongozi wa mashirikisho ya soka barani Afrika hawataki kuachia uongozi mara tu wanapoingia madarakani. Je, unadhani ni kwa nini viongozi hawa huwa hawataki kuondoka? Baadhi ya wapenzi wa pesa wanadhani ni fedha na mamlaka. Lakini je, hizi ni sababu za kutosha kwa kiongozi wa shirikisho kuendelea kuwa madarakani mwaka nenda mwaka rudi? Je, wewe binafsi una maoni gani kuhusu suala hili? Unaweza kutoa maoni yako kwenye BBC Ulimwengu wa Soka kwa kutuandikia ujumbe mfupi wa maandishi, yaani text message au sms, ukitumia nambari hii: + 44 7786 202 005. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||