|
Kimasomaso
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Kuanzia makala ya wiki hii kipindi Kimasomaso kinamulikia utamaduni wa jadi wa jamii za Afrika mashariki na kati – na iwapo
tamaduni hizo zinakifaa kizazi cha sasa au la. Tunaanza kwa kuangazia tamaduni wa jamii ya wa-swahili iishio katika mwambao
wa pwani ya Afrika mashariki. Nayo ni unyago – inayofanyiwa wasichana -- na ile ya jando, inayofanyiwa vijana wa kiume.
Elimu yetu ya jadi ililingana na matakwa na hali halisi ya mazingara yetu. Mazingira-tabia hayo yote yalikuwa na makusudi yake, washiriki, mipaka, lugha au misamiati itumikayo, maadili mema , siasa
zake.
Katika makabila yenye kufuata mila za rika na unyago vijana walitengwa kufundishwa, mithaili ya shule za bweni. Katika makabila yetu yasiyofuata mila za unyago, vijana wa kiume walifundishwa na kuelekezwa na wakubwa wa kiume, kwa mfano, wakati wa kuoga mtoni au ziwani, na masaa ya jioni wakiota moto wakingojea chakula cha jioni, na kadhalika. Hata hivyo kumekuwa na maswali mengi juu ya usiri unaowekewa utamaduni huu hasa kwa watoto wa kike, je nini hasa huendelea pale wanapotengwa wasichana hawa? Je, ni kweli kuwa wao hufunzwa kushiriki ngono? Na iwapo ndio, basi wao hufunzwaje bila ya kuwachochea kuanza ngono mapema?
Tuma maoni au maswali yako kupitia kimasomaso@bbc.co.uk, au tuma text message kwa namba hii + 44 77 86 202 005, au tuandikie barua kwa kutumia sanduku la barua 58621, Nairobi.
|
VIUNGO VYA MTANDAO WA HAPA HAPA
Kuhusu Kimasomaso29 Januari, 2009 | Vivutio
Shughuli za Kimasomaso29 Januari, 2009 | Vivutio
Masimulizi ya washiriki06 Januari, 2009 | Vivutio
Ukweli wa mambo29 Januari, 2009 | Vivutio
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||