Gaza:Makubaliano ya saa 12 yaheshimiwa

  • 26 Julai 2014
Kiongozi wa Hamas na mwenzake wa Israel

Serikali ya Israel na wapiganaji wa Hamas wameanza kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita kwa masaa 12 katika eneo la Gaza kutokana na maswala ya kibinidaamu.

Taarifa ya Israel imesema kuwa raia wa Palestina katika eneo la Gaza ambao walikuwa wameonywa kuondoka katika makaazi yao wasithubutu kurudi na kwamba Israel italipiza kisasi iwapo itashambuliwa.

Hatahivyo Israel imesema kuwa itaendeleza mashambulizi yake kuharibu mahanadaki yanayotumiwa na wapiganaji wa Hamas katika masaa hayo

Awali serikali ya Israel ilikataa makubaaliano ya kusitisha kwa mda mrefu yaliopendekezwa na waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry .

Bwana Kerry amesema ataendelea kushirikiana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ili kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita ya siku saba.

Bwana Ban amesema kuwa vita vinavyoendelea vinaonyesha wazi kwamba hakutakuwa na suluhu ya kijeshi na kwamba uzuiaji wa Gaza ni sharti usitshwe.

Zaidi ya raia mia nane wa palestina wameuawa pamoja na wa Israel zaidi 30.