BBC navigation

27 wauawa katika vita vya kikabila DRC

Imebadilishwa: 7 Juni, 2014 - Saa 15:44 GMT

Takriban watu 27 wakiwemo watoto na wanawake wameuawa katika mapigano Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Yanaaminika kuwa mapigano ya kikabila.

Walioshuhudia mapigano hayo wanasema kuwa miongoni mwa waliouawa walikuwa wanawake 14 na watoto 8 baadhi yao wakiwa ndani ya kanisa ambamo walikuwa wanalala

Waathiriwa wote walikuwa watu wa kabila la Bafuliru.

Haijulikani nani aliyetekeleza mashambulizi hayo lakini eneo hilo limeshuhudia mgogoro kati ya watu wa kabila la Bafuliru na Barundi

Mwandishi wa shirika la habari la Reuters alisema kuwa waathiriwa walipigwa risasi , kudungwa visu au kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba zao.

Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Kivu Kusini, Jean-Julien Miruho aliambia shirika la habari la Agence France Presse kuwa uvamizi huo ulikuwa uvamizi wa kulipiza kisasi kwa wizi wa mifugo.

Taarifa zaidi

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.