BBC navigation

Nigeria yaahidi kuwatafuta wanafunzi

Imebadilishwa: 25 Aprili, 2014 - Saa 12:04 GMT

Wazazi wa wanafunzi walijaribu kwenda msituni wenyewe kuwatafuta watoto wao wakilaumu serikali kwa kujikokota

Juhudi za kuwaokoa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo la Boko Haram, zimepewa kipaombele katika mkutano wa serikali kuhusu hali ya usalama nchini Nigeria.

Mkutano huo uliongozwa na Rais Goodluck Jonathan.

Mkutano wenyewe uliodumu kwa saa sita, ulihudhuriwa na maafisa wakuu wa usalama , mawaziri na maafisa wakuu wa serikali kutoka pande zote..upande wa waisilamu na wakristo.

Wanaouhudhuria walikubaliana kuwa mgogoro kati ya wanajeshi wa serikali na kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram, Kaskazini mwa nchi sio vita vya kidini bali vita dhidi ya raia wa Nigeria.

Juhudi za serikali kupambana na Boko Haram Nigeria zimeonekana kupatwa na changamoto nyingi

Wanafunzi zaidi ya miambili walitekwa nyara wiki jana na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram na kuwapeleka msituni.

Baadhi ya wasichana hao walifanikiwa kutoroka lakini wengine wengi wangali wanazuiliwa.

Wapiganaji hao wamesababisha vifo vya maelfu ya watu nchini humo wakidai kuwa wanapigania kile wanachosema ni misingi ya dini ya kiisilamu.

Kundi hilo pia lilikiri kufanya shambulizi baya katika kituo cha basi mjini Abuja wiki jana ambapo zaidi ya watu 70 waliuawa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.