BBC navigation

Australia yadadisi picha za Satelite

Imebadilishwa: 20 Machi, 2014 - Saa 15:27 GMT

Harakati za kutafuta ndege ya Malaysia

Australia inadadisi picha za Satelite za vitu viwili vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege iliyopotea ya Malaysia.

Nchi hio inashirikiana na Norway, New Zealand na Marekani kutafuta mabaki hayo.

Upepo mkali na mvua zilitatiza juhudi hizo hii leo na kusababisha shughuli hiyo kusitishwa. Hata hivyo msako huo utaendelea siku ya Ijumaa.

Picha za Satelite za kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege

Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott mapema leo aliambia bunge la nchi hio kuwa picha zilizonaswa na mitambo ya Satelite ya nchi hio baharini, zilionekana kama vipande viwili vya mabaki ya ndege hiyo.

Kipande kimoja kilikuwa na urefu wa mita 24.

Bwana Tony Abbott,aliambia bunge kuwa hii ni taarifa mpya na iliyothibitishwa.

Lakini maafisa wakuu nchini Malaysia wametahadharisha kuwa mabaki hayo huenda sio ya ndege yake, ambayo ilipotea siku kumi na tatu zilizopita ikiwa imewabeba watu 239 kuelekea Beijing.

Mabaki hayo yalionekana umbali wa kilomita elfu mbili miatano Kusini Magharibi mwa mji wa Perth.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.