BBC navigation

Wachimba migodi wahofia kukamatwa

Imebadilishwa: 18 Februari, 2014 - Saa 07:17 GMT

Mmoja wa wachimbaji akiokolewa kwenye mgodi uliotelekezwa.

Kundi la wachimbaji migodi haramu waliookolewa kutoka mgodi uliotelekezwa nchini Afrika Kusini na maafisa wa uokoaji wanatarajiwa kufika kizimbani hivi leo.

Wachimbaji migodi hao 11 walitumia ngazi iliyotupwa ndani ya mugodi huo kujinasua siku ya jumatatu.

Wote 22 walikamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vinasema takriban wachimba migodi wengine 200 bado wamenasa katika mgodi huo lakini wamekataa kuokolewa wakihofia kukamatwa na polisi. Baadhi yao wanatoka katika mataifa jirani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.