BBC navigation

Marekani na EU njia panda kuhusu Ukraine

Imebadilishwa: 7 Februari, 2014 - Saa 07:19 GMT

Nuland na Rais Yanukovich

Tofauti za sera kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya kuhusiana na mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine zimebainika wazi baada ya kuibuka mazungumzo ya siri baina ya maafisa wawili wakuu wa kidiplomasia Kiev.

Mazungumzo yanayotajwa kuwa yalinaswa kisiri kati ya wanadiplomasia wawili wakuu wa Marekani wakizungumzia mstakabali wa Ukraine baada ya tandabelua la kisiasa yameiwacha marekani ikionekana Mshari.

Katika mazungumzo hayo yaliyonaswa kisiri naibu waziri wa wa mambo ya nje wa Marekani, Sauti ya Victoria Nuland, anasikika akimwambia balozi wa Marekani nchini Ukraine, Geoffrey Pyatt, kuwa hamtaki aliyekuwa mwanamasumbwi, Vitali Klitschko katika serikali ijayo badala yake anasikika akisema 'Yats', akiashiria Arseniy Yatsenyuk ndiye anayepaswa kuwa na usemi mkubwa kutokana na tajriba yake kuu ya kiuchumi na Utawala.

''Yats ndiye anayepaswa Kuingia serikalini na afanye mazungumzo na Klitschko mara nne kila juma''

Nuland anasikika akiitusi Umoja wa Ulaya na kusema kuwa Umoja wa Mataifa ndiyo unaopasawa kuwa na usemi kuhusiana na hali ilivyo Ukraine kwani Kulinga naye 'Umoja wa mataifa ndio unapaswa kusaidia makundi ya upinzani kushikamana ''

Taharuki Kiev

Msemaji katika wizara ya mashauri ya kigeni ya marekani Jen Psaki, hakupinga uhalali wa taarifa hizo.

Msemaji wa ikulu ya White House Jay Carney, amesema kuwa taarifa hizo ziliwekwa kwenye mtandao wa Twitter na afisa wa Urusi.

Kashfa hii ya kidiplomasia inatukia baada mshauri mkuu wa Rais Putin kulaumiwa na Marekani kwa kujiingiza katika siasa Ukraine.

Sergei Glazyev ameilaumu Marekani kwa kutoa mamilioni ya dola kwa vyama vya upinzani mbali na kuwakabidhi silaha.

Mshauri huyo wa Putina anasema hatua ya Marekani kuingilia maswala ya ndani ya Ukraine kimsingi inaipa Urusi uhuru na haki ya kuingilia kati.

Rais Putin anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake wa Ukraine Viktor Yanukovych wakati wa michezo ya olympiki ya msimu wa baridi huko in Sochi .

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.