BBC navigation

Oxfam yamtema Scarlet Johanneson

Imebadilishwa: 30 Januari, 2014 - Saa 13:57 GMT

Scarlet alikuwa balozi wa kimataifa wa Oxfam

Muigizaji wa kike wa Hollywood Scarlett Johansson amekomesha miaka yake minane kama balozi wa shirika la misaada ya kibinadamu la Oxfam.

Shirika hilo linamkosoa kwa kuunga mkono kampuni moja ya Israel inayoendesha shughuli zake katika eneo linalokaliwa na walowezi la Ukingo wa Magharibi.

Oxfam linasema kuwa uhusiano wa mwanasanaa huyo na Kampuni ya SodaStream iliyo na kiwanda katika eneo linalokaliwa na walowezi wa kiyahudi haiandamani na majukumu yake ya kuwa balozi wa kimataifa wa Oxfam

Hivi majuzi Scarlett Johansson alisaini mkataba na kampuni hiyo ya SodaStream na ataonekana katika matangazo ya kampuni hiyo wakati wa sherehe za American Superbowl mnamo siku ya Jumapili.

Oxfam inakataa biashara zozote kutoka kwa walowezi wa kiisrael, huku ikisema ni kinyume kulingana na sheria za kimataifa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.