BBC navigation

Waziri Mkuu wa Latvia ajiuzulu

Imebadilishwa: 27 Novemba, 2013 - Saa 14:44 GMT

Valdis Dombrovskis,waziri mkuu wa Latvia

Waziri Mkuu wa wa Latvia, Valdis Dombrovskis, amejiuzulu kufuatia kuporomoka kwa jengo moja nchini humo, Alhamisi iliyopita na kusababisha watu wapatao hamsini kuuawa.

Bwana Dombrovskis amesema amekubali kuwajibika kisiasa kutokana na mkasa huo ambapo paa ya duka moja kubwa la bidhaa katika mji mkuu, Riga, lilipinda na kuporomoka.

Polisi wameanzisha uchunguzi wa kihalifu kubaini kama taratibu za ujenzi wa jengo hilo zilizingatiwa au la; bustani ilikuwa ikijengwa juu ya paa la jengo hilo la maduka wakati ajali hiyo ikitokea.

Latvia imekuwa na siku tatu za maombolezo kuwakumbuka waathirika wa janga hilo, ambalo ni baya kuwahi kutokea nchini Latvia, tangu nchi hiyo ijipatie uhuru wake mwaka 1981.
Kujiuzulu kwa Bwana Dombrovskis, ambaye ameiongoza Latvia katika kipindi cha mgogoro wa kiuchumi, kumekuja wiki kadhaa kabla ya nchi hiyo kujiunga na umoja wa Ulaya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.