BBC navigation

Putin awaasa wamarekani kuhusu Syria

Imebadilishwa: 12 Septemba, 2013 - Saa 06:20 GMT

Rais Vladmir Putin ni mshirika mkubwa wa serikali ya Syria

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa ombi la moja kwa moja kwa raia wa Marekani kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Syria.

Katika tahariri ya gazeti la New York Times, Putin ameonya kwamba shambulio lolote la jeshi la Marekani dhidi ya Syria litasababisha kuzuka kwa wimbi jipya la ugaidi na huenda likasababisha kubadilika kwa mfumo mzima wa sheria na utulivu wa kimataifa.

Amesema kuwa mamilioni ya watu wanaiona Markani kama mfano wa taifa lenye demokrasia lakini hutumia sana nguvu.

Tahariri hiyo inachapishwa siku ambapo maafisa wakuu wa Marekani na Urusi wanatarajiwa kujadili yaliyomo katika pendekezo la Urusi la kudhibiti kimataifa silaha za kemikali za Syria.

Wakati huo huo kumekuwa na mapigano mazito nchini Syria katika kujaribu kuudhibiti mji mkongwe wa kikristo Maaloula, licha ya taarifa zinazoeleza kwamba kikosi cha serikali kiliudhibiti kutoka kwa wanamgambo wenye misimamo mikali ya dini ya kiislamu.

Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa rais wa Syria Bashar al-Assad, imependekeza kudhibiti silaha za kemikali zilizo nchini Syria.

Japan iliwahi kutumia silaha za kemikali dhidi ya wachina mwaka 1930, Mussolini akatumia silaha hizo nchini Ethiopia wakati wa vita vya pili vya dunia huku jeshi la Misri likitumia silaha hizo nchini Yemen miaka ya sitini.

Lakini yote haya hayawezi kufananishwa na kilichotokea eneo la Halabja. Mwezi Machi mwaka 1988, aliyekuwa rais wa Iraq Saddam Hussein aliamuru kutumiwa kwa gesi ya sumu dhidi ya wakurdi na kuwaua watu zaidi ya 5,000 papo hapo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.