Bomu lauwa watu kadha mpakani Uturuki

  • 11 Mei 2013

Wakuu wa Uturuki wanasema watu kama 18 wamekufa kwenye mripuko wa bomu lilotegwa kwenye gari katika mji ulio karibu na mpaka wa Syria.

Mfuga kondoo apita karibu na kambi ya wakimbizi wa Syria Reyhanli, Uturuki

Walioshuhudia tukio hilo katika mji wa Reyhanli, kilomita chache kutoka kituo muhimu cha mpakani, wanasema kulitokea miripuko kama mine kati-kati ya mji.

Wakimbizi wengi kutoka vita vya Syria wamepata hifadhi katika mji huo.

Haijulikani nani alihusika na shambulio hilo.

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu alionya kuwa Uturuki iko tayari kujihami, mtu asijaribu kuipima nguvu.

Eneo la mpakani limewahi kushambuliwa kwa mizinga kutoka upande wa Syria.