BBC navigation

Bomu kanisani Arusha lauwa mtu mmoja

Imebadilishwa: 5 Mei, 2013 - Saa 18:46 GMT


Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa mtu mmoja amekufa kwenye mripuko uliotokea katika ufunguzi wa kanisa la Katoliki la Olasiti, kwenye kitongoje cha Arusha, Tanzania.

Polisi wakiwasili kwenye kanisa baada ya mripuko

Watu kama 50 wamejeruhiwa.

Makamo wa rais wa Tanzania, Dr. Mohamed Gharib Bilal amewasili Arusha kwenda kupeleka pole ya serikali kwa viongozi wa kanisa na majeruhi.

Dr. Bilal alisema serikali ya Tanzania itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa inawapata watu waliohusika na mripuko huo.

Mtu mmoja amekamatwa lakini haikuelezwa ni nani au kama amehusika na kundi lolote.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.