BBC navigation

Maporomoko yasababisha vifo Indonesia

Imebadilishwa: 25 Machi, 2013 - Saa 09:23 GMT
Waokoaji nchini Indonesia

Waokoaji nchini Indonesia

Watu sita wamefariki na wengine 18 hawajulikani walipo baada ya ardhi kuporomoka katika kisiwa cha Java nchini Indonesia.

Mamia ya polisi, wanajeshi na umma wamekuwa wakichimba magofu wakiwatafuta manusuru.

Kama ilivyo desturi nchini Indonesia, mvua kubwa ya msimu husababisha maporomoko ya ardhi kila mwaka.

Brazil

Na huko Brazil pia, mvua kubwa imesababisha mafuriko na kuvuruga maisha ya wakaazi wa jimbo la Rio de Janeiro.

Katika mji wa Angra dos Reis, watu 3,000 walikatiwa mawasiliano wakati daraja muhimu linalowaunganisha na miji mingine lilipokatika.

Miporomoko miwili ya ardhi pia iliwazuia watu kufika mjini humo.

Maporomoko ya ardhi yamewauwa makumi ya watu katika majuma kadhaa yaliyopita eneoni humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.