BBC navigation

Papa Francis 1 siku ya kwanza

Imebadilishwa: 14 Machi, 2013 - Saa 08:32 GMT

Kazi yaendelea Vatican

Siku yake ya kwanza ofisini kama Papa mtakatifu wa kanisa Katoliki, Papa Francis 1 tayari anaanza kazi. Papa anatarajiwa kuwateua wafanyikazi wakuu watakaohudumu katika Vatican chini ya uongozi wake. Ameanza siku yake kwa maombi ya kibinafsi katika hekalu ya mtakatifu Maria Maggiore mjini Rome.

Baadaye Papa atafanya misa ya sherehe katika kanisa la Sistine.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa uteuzi atakaofanya Papa Francis, utatizamiwa kama ishara ya mageuzi katika uongozi uliozongwa na kashfa nyingi na pia utaonyesha mwelekeo anaonuia kuchukua kwa kanisa hilo.

Baadaye wikendi ijayo, Papa mpya anatarajiwa kukutana na vyombo vya habari vya dunia katika mkutano maalum.

Na Jumapili, ataongoza misa yake ya kwanza kama papa. Hata hivyo yeye mwenyewe atatawazwa rasmi kuwa Papa Francis 1, siku ya Jumanne.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.